Deuteronomy 6:6-8

6 aAmri hizi ninazokupa leo zitakuwa katika moyo wako. 7 bWafundishe watoto wako kwa bidii. Nena kuhusu amri hizi uketipo nyumbani na wakati utembeapo njiani, ulalapo na uamkapo. 8 cZifunge kama alama juu ya mkono wako, na uzifunge juu ya paji la uso wako.
Copyright information for SwhKC